Uliniahidi penzi,
Si jana, si juzi,
Si leo, si kesho,
Wangu kidosho,
langu penzi hadi mwisho.

Uwe wangu wa milele,
Nikatae nipe kiwewe,
Nkubali nipige kelele,
kwa nguvu uskie wewe.

Napo sasa naamua,
Kutoka kwetu kutimua,
Karibu nawe naja,
Kutimiza langu haja.

Wazaziyo nawajia,
Hoja langu kuwaambia,
Nao mkazo nalitia,
Uwe wangu malikia,
Milele kwa hii dunia.

Hudhaifah Siyad

http://www.poemhunter.com/poem/mapenzi-moto-moto-swahili-language/