WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika za kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.<br />Majaliwa aliyasema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika kuhusu mkataba huo akimwakilisha Rais John Magufuli Jijini Kigali ambapo alisema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo.