Hatimaye mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wa kwanza wa ligi hiyo msimu huu baada ya kucheza michezo 28 bila kupoteza.

Simba wamefungwa bao 1-0 na Kagera Sugar, kwenye mchezo uliopigwa dimba la Taifa Dar es Salaam na kushuhudiwa na Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Bao pekee la Kagera limefungwa dakika ya 85 ya mchezo na Edward Christopher huku Simba wakipoteza mkwaju wa penati uliopanguliwa na kipa wa Kagera, Juma Kaseja.

Baada ya mchezo huo Rais Magufuli ameikabidhi Simba kombe la ubingwa wa VPL msimu wa 2017/18 huku akieleza kutoridhishwa na kiwango alichoshuhudia