Mabao matatu yamefungwa ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza na kuifanya Yanga iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.<br /><br />Mabao ya Yanga yalifungwa na Matheo Anthony dakika ya 19 na Maka Edward dakika ya 39 huku Ruvu shooting wakipata bao lao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Khamis Mcha.<br /><br />Mchezo huu ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 baada ya Isa Kanduru kuifungia Ruvu Shooting bao la kusawazisha dakika ya 46 ya mchezo.