Ubomoaji wa jumba la Airgate Mall al -maarufu Tajj Mall ulioanza hapo jana uliendelea hii leo baada ya sehemu ya nyumba hiyo kuanguka wakati wabomoaji walikuwa wakiondoa mabaki ya jengo hilo.<br /><br />Mmiliki wa jumba hilo Ramesh Chandaria Gorasia ambaye hakufika eneo hilo ametishia kuelekea kortini kuwashtaki wabomoaji hao licha ya kupewa ilani ya kuhama mwezi mmoja uliopita.