Idadi ya watu walioangamia nchini Tanzania kwenye mkasa wa ferry kuzama katika ziwa Victoria imefikia watu 126.<br />Ferry hiyo ya John Magufuli ilizama Alhamisi jioni ilipokuwa ikitoka kisiwa cha Bugorora kuelekea kisiwa cha ukara ikiwa imebeba takriban abiria 300, wengi wao wakiwa wafanyibiashara.<br />Rais Uhuru Kenyatta ameelezea kusikitishwa kwake na mkasa huo na kumpa pole rais John Magufuli na raia wa Tanzania kwa niaba ya wakenya.