YANGA imetwaa taji la Ngao ya Jamii mbele ya watani zao wa jadi Simba katika mchezo uliokuwa na mvuto mkubwa.<br />Bao la ushindi limepachikwa na Fiston Mayele kwa shuti kali ambalo lilimzidi ujanja Aishi Manula kipa namba moja wa Simba.<br /><br />Kiungo mkata umeme Taddeo Lwanga alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.